Moja ya nyumba za asili za wanyakyusa

Historia inasema kwamba asili ya Wanyakyusa ni mkoani Morogoro. Kabila hilo likitokana na kabila la Waluguru. Hili hasa ndilo chimbuko la Wanyakyusa.

Nyani aina ya kipunji wanaopatikana mlima Rungwe tu.

Katika mlima rungwe kuna viumbe hai mbali mbali kama ndege na wanyama. Moja ya wanyama wanaopatikana katika mlima rungwe ni nyani ambapo kuna aina moja ya nyani wanaopatikana mlimani hapo tu ambao wanajulikana kama kipunji.

AGA KHAN YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KWA HOSPITALI ZA HALMASHAURI 4 ZA MBEYA‏

Mwenyekiti wa kamati ya afya Aga Khan Mbeya (kushoto)Sultan Thawer, akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro kabla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya tiba kwa Halmashauri nne za Mkoa wa Mbeya..

BIOLANDS YAKABIDHI MSAADA WA AMBULANCE NISSAN PATROL KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA KYELA.

Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Malenga akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Gari la Wagonjwa walilokabidhiwa na kampuni ya Biolands , akisaidiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Seif Mhina .

KERO KATIKATI YA JIJI LA MBEYA

KERO KATIKATI YA JIJI LA MBEYA: MACHINGA WAJIACHIA WAPANGA BIDHAA MPAKA BARABARANI , WAHUSIKA WAMEUCHUNA, JE MAPATO HAYA YANAENDA WAPI? NA NI SAHIHI HAWA WATU KUWA HAPA?

Monday, November 3, 2014

HISTORIA YA WANYAKYUSA

HISTORIA YA WANYAKYUSA
Historia inasema kwamba asili ya Wanyakyusa ni mkoani Morogoro. Kabila hilo likitokana na kabila la Waluguru. Hili hasa ndilo chimbuko la Wanyakyusa.

Inasemekana kwamba mwindaji mmoja wa Kiluguru alitembea peke yake porini bila ya kuongozana na mtu mwingine. Alitembea hadi akafika maeneo ya Kabale huko Suma, Tukuyu wilayani Rungwe. Akiwa huko, akaendelea na kazi yake ya uwindaji.
Baadaye akatokea Mzulu mmoja kutoka Afrika Kusini aliyekuwa na binti yake. Akafika maeneo alikokuwa akiishi yule mwindaji Mluguru, naye akapiga kambi hapo Kabale, wakaungana katika maisha ya uwindaji.

Ikawa kila yule Mluguru akitoka asubuhi kwenda kuwinda, alikuwa akifanikiwa kurejea nyumbani na wanyama wakati rafiki yake wa Kizulu alikuwa akirudi mikono mitupu.

Kutokana na hali hiyo, Mluguru akageuka kuwa mfadhili wa Mzulu, kwa kutoa misaada mara kwa mara, na kwa kulipa fadhila hizo, akamwoza bintiye kwa Mluguru.

Akamwoa na maisha yakaendelea huku nyumbani kwa mwindaji wa Kiluguru na mkewe binti wa Kizulu, kukiwa hakukosekani nyama kama kitoweo.

Kwa sababu ili kuihifadhi nyama ilibidi kwanza ibanikwe, basi kitendo hicho kilisababisha harufu nzuri ya kitoweo kile kusambaa eneo kubwa na kufika hadi ukweni kwake nyumbani kwa Mzulu. 
 Moja ya nyumba za asili za wanyakyusa

Ndipo Mzulu yule akawa anasema mara kwa mara: “Pale panatoa kyusi kila siku” akimaanisha moshi kwa lafudhi ya lugha ya kwao.

Mazoea ya kutamka ‘kyusi’ kila siku, yakaligeuza neno ‘kyusi’ na sasa likawa linatamkwa ‘kyusa’, baadaye ‘kyusa’ ilipozidi kutamkwa kwa mara nyingi, nayo pia ikabadilika bila kukusudia ndipo watu walipokuwa wakimwita Mluguru ‘Mnyakyusa’, kwa kuwa moshi ukiambatana na harufu ulikuwa ukitokea ndani ya nyumba yake na kusambaa.

Kwa hiyo, tangu hapo na kutokana na jina hilo alilopewa kwa ajili ya mazoea ya kukosea kutamka kitu, hata watoto wake pia waliozaliwa na Mluguru na mkewe Mzulu, wakawa wakiitwa ‘Wanyakyusa’.

Hiyo ndiyo asili na chimbuko la kabila la Wanyakyusa, na kwa kuwa Mnyakyusa alikuwa tayari ana asili ya pande mbili - wakati baba akiwa na asili ya Kiluguru na mama Mzulu wa ‘kwa Madiba’.

Na hata uchifu ukaanzia mahali pale palipokuwa panaitwa Kabale, na yule Mluguru aliupata uchifu kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa mwanzilishi na mkazi wa kwanza wa eneo lile na ndiye aliyekuwa anafahamika zaidi.

Mavazi yao

Kwa upande wa mavazi, Wanyakyusa walikuwa wakivaa mavazi yaliyokuwa yakijulikana kama ‘Lyabi’, Ni mavazi ya kwanza kwa kabila yakivaliwa enzi za utumwa. Mavazi haya ni yale yanayofunika maeneo ya siri pekee, na kwa wale ‘waheshimiwa’, kidogo basi wao walivaa vazi lililokuwa likiitwa ‘kikwembe’ au ‘kilundo’.

Mavazi haya yaliyovaliwa kwa mtindo kama lubega, ndiyo yaliyomtambulisha na kumtofautisha mhusika mbele ya jamii.

Ngoma yao

Ngoma iliyokuwa ikichezwa na Wanyakyusa enzi hizo, ilikuwa ni ya kuchezea mikuki na mara nyingi ngoma hiyo ilikuwa ikichezwa wakati wa msiba.

Lakini ngoma za kawaida zilizokuwa zikichezwa pasipo kutumia mikuki na wakati wa sherehe na shughuli nyingine, ni ‘Ipenenga’. Hii mara nyingi ilikuwa ikichezwa na watu ‘wastahiki’ tena kwa madaha na maringo ya hali ya juu. Hata machifu walikuwa wakiicheza sana ngoma hii.

Chakula chao

Chakula chao kikuu na ambacho Mnyakyusa angeonekana kuwa amemkarimu mgeni, si kingine bali ni dizi zinazomenywa na kupikwa maarufu kama ‘mbalaga’.

Mnyakyusa halisi kama atakula chakula lakini akakosa ‘mbalaga’ hujiona kama bado hajakamilisha mlo, ingawaje siku hizi kuna mabadiliko fulani ambayo wengi hupendelea ugali na wali; lakini bado asili ya chakula chao hawawezi kuibadilisha kamwe.

Na ni lazima chakula kama ‘kande’ kipikwe kwenye tukio la msiba uwao wote, kama shughuli za msiba zitakwisha pasipo kupikwa chakula hicho chenye mchanganyiko wa mahindi na maharage; msiba huwa haujakamilika hata kama wafiwa ni watu wenye kujiweza kifedha zaidi lakini ni lazima kande zitapikwa japo kiasi.

Utamaduni wao
Kwa kawaida Wanyakyusa hawana mambo ya unyago kama ilivyo kwa baadhi ya makabila hapa nchini. Wao hawapendelei kabisa mila na desturi za kuwaweka mabinti ndani au kuwafanyia mambo yoyote ya tohara.

Hii ni pamoja na upande wa vijana wa kiume ambao nao hawafanyiwi ya tohara kama makabila mengine isipokuwa tu kwa upande wa vijana wa kiume mara tu wanapotimiza umri wa miaka 13 na kuendelea.

Hawa wazazi wao wa kiume huwatengea eneo ambalo kijana hutakiwa kujifunza kujitegemea akiwa bado mbichi. Hapo hutakiwa kuwa na kibanda chake na kuhama kutoka nyumba moja na wazazi wake
Chanzo: SAUTI YA VIJANA BUSOKELO

MLIMA RUNGWE



Mlima rungwe ni mlima ulipopo katika wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, Inaaminika kwamba mlima huu ulitokana  na volcano iliyozimika kusini kusini magharibi mwa Tanzania,  Ikikadiriwa ya kwamba mlipuko wake wa mwisho ulitokea mnamo miaka 2000 hadi 5000 iliyopita. Ukiwa na kimo cha 2960 m ni mlima mkubwa kusini mwa Tanzania na ni wa tatu kwa ukubwa Tanzania
 Mlima Rungwe

 Mlima Rungwe ukionekana kwa mbali kama picha ilivyochukuliwa kutoka The green city Profile

Mlima unasimama juu ya ncha ya kaskazini ya Ziwa nyasa. Upande wa kusini-mashariki wa mlima hupokea usimbishaji wa 3,000 mm kwa mwaka ambao ni juu kabisa katika Tanzania.

Mazingira ya mlima ni nchi yenye rutba na kilimo. Rungwe ni eneo la Wanyakyusa.Jina la mlima limekuwa pia jina la wilaya ya Rungwe

 Katika mlima rungwe kuna viumbe hai mbali mbali kama ndege na wanyama. Moja ya wanyama wanaopatikana katika mlima rungwe ni nyani ambapo kuna aina moja ya nyani wanaopatikana mlimani hapo tu ambao wanajulikana kama kipunji.
Nyani aina ya kipunji wanaopatikana mlima Rungwe tu

 


Ukiwa juu yam lima rungwe unaweza kuliona ziwa nyasa vizuri pamoja na mbuga ya wanyama kitulo. Upande wa kusini mwa mlima utaona ziwa nyasa na upande wa mashariki utaona bonde la kitulo.
 Ziwa Nyasa
Kitulo National Park

HIKI NDO KIMONDO KILICHODONDOKA MBOZI TANZANIA

Kimondo ambacho kilidondoka kutoka angani huko Mbozi mbeya karibu na mji wa vwawa.Kinakadiriwa kuwa na uzito wa tani 12 na kilianguka katika mlima wa mlenje

Kimondo hicho ni kimoja kati ya vimondo 10 vinavyojulikana duniani na kina urefu wa mita 3.3 na urefu wa mita 1.63 na kimo cha 1.22.

Kwa upande wa umbile kimondo hichi kiko tofauti na vimondo vingine vinavyopatikana ulimwenguni kwa sababu kimondo hichi ni hasa kwa chuma. Chuma kimechukua asilimia 90.45 na nikel asilimia 8.69, sulfuri asilimia 0.01 na fosfori asilimia 0.11 ya masi yake

Maporomoko ya Malasusa

Malasusa falls
Maajabu mengi yaliyopo Tukuyu mkoani mbeya ni maporomoko ya Malasusa . ukiwa unaelekea kwenye maporomoko ya Malasusa utasikia
maporomoko  kwa mbali kabla hujafika kwenye maporomoko yenyewe na ni moja kati ya maporomoko mazuri katika ukanda wa nyanda za juu kusini
 Maporomoko ya Malasusa kama picha ilivyochukuliwa na Emwandosya

MKURUGENZI, WANAHABARI NA WANANCHI MBEYA, KUISAFISHA MBALIZI

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbeya, Upendo Sanga
MKURUGENZI wa halmashauri ya Mbeya, Upendo Sanga, baadhi ya wanahabari mkoani Mbeya, wananchi na wakuu wa idara za Halmashauri hiyo, wanatarajia kuongoza kampeni endelevu ya kuuweka safi mji wa Mbalizi wilayani humo na kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira.


Kampeni hiyo ya usafi, inaratibiwa na kikundi cha Vijana wanaofanya kazi ya kutunza na kuhifadhi mazingira kwa kujitolea mkoani hapa, wanaojulikana kwa jina la Vijana wazalendo Mbalizi(UVIWAMBA).


Akizungumza na waandsishi wa habari jana, mratibu wa kikundi hicho, Gordon Kalulunga, alisema kuwa, itakuwa mara ya pili kwa Mkurugenzi huyo na baadhi ya waandishi wa habari kuungana na juhudi za vijana wanaojitolea kufanya usafi katika mji huo.


“Ni faraja kubwa sana kwetu kuona Halmashauri yetu inaungana nasi katika kutimiza wajibu wetu kwa taifa, hasa tunapoona Mkurugenzi na waandishi wa habari wanakuja huku chini na kuona umuhimu wa kutoa support kwa kada ya watu tunaoamua kujitolea” alisema Kalulunga.


Alisema usafi huo utafanyika katika eneo la makao makuu ya Kanisa la Uinjilisti Tanzania mpaka eneo la stendi ya Umalila, na kuhitimishwa kwa kubadilishana mawazo endelevu ya usafi katika mji huo wa Mbalizi kati ya wananchi watakaojitokeza na wageni watakaoongozwa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo.


Naye makamu Mwenyekiti wa kikundi hicho, Ayas Yusuph, alisema kikundi chao kinafanya usafi kila siku ya Juma mosi ya juma kwa kushirikiana na baadhi ya wananchi wa mji huo.


“Mkurugenzi kuungana nasi ni jambo kubwa sana ambalo linatuongezea hamasa ya kuendelea kujitolea na hivi sasa tayari tumebandika matangazo kwa ajili ya kuwaeleza wananchi wenzetu kuwa kila mmoja siku hiyo afanye usafi kwa hiari katika makazi na maeneo anayofanyia kazi’’ alisema Ayasi.


Kwa upande wake Mkurugenzi Upendo Sanga, alisema, ataungana na vijana hao pamoja na baadhi ya wakuu wa idara ya mazingira, kufanya usafi katika mji huo ambao ni kioo cha wilaya na mkoa wa Mbeya kwa wageni wanaotumia usafiri wa ndege wa kimataifa wa Songwe.


“Nitashiriki katika zoezi hilo la usafi siku ya Jumamosi. Ni wajibu wangu na wananchi wote, maana Mbalizi ni kioo cha mkoa wa Mbeya kupitia uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Songwe, ambao upo katika wilaya yetu na mgeni yeyote anayetaka kwenda katikati ya Jiji la Mbeya, lazima apite Mbalizi” alisema Upendo Sanga.

 AKISHIRIKI KUZIBUA MIFEREJI NA VIJANA WA MBALIZI AMBAO WAMEJITOLEA KUFANYA USAFI KATIKA MJI HUO.

 AKIWA NA VIJANA ENEO LA KAZI MBALIZI MWAKA JANA 2013.

Kushirki katika kazi hiyo ya usafi kwa Mkurugenzi huyo, kutakuwa kwa awamu ya pili, ambapo awali mwaka jana, alishiriki katika kuzibua baadhi ya mitaro iliyokuwa imeziba katika stendi kuu ya wilaya hiyo, iliyopo eneo la Tarafani katika mji wa Mbalizi.


Kwa sasa Serikali, inaendelea kukamilisha ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami katika mji huo.

MANGULA KUKABIDHIWA KADI ZA CCM ILEJE MBEYA



BAADHI ya wanachama wa Chama Cha Mpinduzi(CCM) Wilayani Ileje mkoani Mbeya, wamejipanga kumkabidhi kadi za chama hicho, Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Philipo Mangula, ambaye pia ni mlezi wa chama hicho mkoa.

Hatua hiyo inakuja baada ya siku chache, kamati ya siasa ya wilaya hiyo, kusimamishwa na kamati ya siasa ya mkoa, kutokana na maelewano hasi ya baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya na hatimaye kufikia hatua ya kufunga ofisi ya wilaya.

Taarifa za uchunguzi zinaonyesha kuwa, makundi yanayosigana kuhusu nafasi ya Ubunge na Urais mwakani 2015, ni moja ya vyanzo vya mzozo huo.

Wanaotajwa kuwa wana nguvu za kuwania nafasi hiyo ni Mbunge wa sasa, Aliko Kibona na Naibu Waziri wa Viwanda, Janet Mbene.

Janet Mbene, anaelezwa kuwa na kundi kubwa wakiwemo baadhi ya wakuu wa idara na watumishi wa serikali wilayani Ileje.

Taarifa zinasema kuwa, Mangula anatarajia kuwasili mkoani Mbeya, na kufanya vikao vya ndani ikiwemo kushughulikia mzozo wa wilaya ya Ileje na Jumatatu atakuwa Jijini Mbeya.

SHETANI KAWEKEZA KWENYE KILA KITU KIZURI




Kila kwenye kitu kizuri, shetani kaweka mguu wake.

(Nazungumzia maadili ya vijana). simu ni moja ya kitu kizuri, lakini shetani kaweka mguu wake kuharibu maadili ya vijana. 

Nilijaribu kujiuliza kuwa kwanini hata sukari na nyama watu wanakatazwa na kuruhusiwa kula matembele? why?

Kila kitu kizuri, shetani amewekeza na kujipachika hapo. Kijana kama una simu na account za fb, ni vema kutumia vizuri. simu nyingi za vijana hazina maadili.

leo hii ukichukua simu ya kijana wa kike/kiume na kuangalia maeneo ya sms inbox na sent, photo na kipengele cha video, utakutana na picha ambazo hazina maadili(picha za kusulubiana) na kuwalisha watu 5000 mikate.

MAKALA UKATILI WA KIJINSIA

UKATILI WA KIJINSIA KATIKA JAMII

   NINI MAANA YA UKATILI WA KIJINSIA 

         Ni kitendo cha ukatili kuhusu jinsia ambacho kinaweza kusababisha madhara / maumivu ama mateso ya kimwili au kisaikolojia kwa mtu ikiwa ni pamoja na vitendo vya kutishia ,kulazimisha kunyima uhuru,bila kujali vimefanyika kisiri ama kwenye kadamnasi".
  NB: ukatili wa kijinsia huhusishwa na ukatili kwa wanawake kwani wao ndio waathirika zaidi wa ukatili.

AINA ZA UKATILI WA KIJINSIA  
 
kuna aina nyingi za ukatili wa kijinsia .


UKATILI WA KUTUMIKA NGUVU

kupigwa makofi ,mateke ,
kuchapwa
kutupia au kupigwa na vitu vya ndani


UKATILIWA KISAIKOLOJIA

kusema mambo yanayomfanya mtu kujisikia mdogo,
kunyanyasa
kusimangwa
kudhalilisha
kuwekwa chini yake,kukuweka mbali na ndugu au marafiki .

UKATILI WA KIUCHUMI

kunyimwa mahitaji muhimu na fedha za kujikimu ,
kunyimwa umiliki wa mali,
kuzuiwa kufanya kazi.


UKATILI WA KIUTAMADUNI NA MILA KANDAMIZI

Ndoa za utotoni .
utakasaji na kurithi wajane ,
Mauaji ya vikongwe.
Ukeketaji


UKATILIWA KINGONO


kubakwa
kulawitiusafirishwaji wa watu wanawake na watoto
kukushika bila ya ridhaa

HALI YA UKATILI WA KIJINSIA TANZANIA

kutokana na taarifa ya demographic health survey 2010 inaonesha tatizo limekuwa , linakuwa na linakithiri katika sehemu zote za tanzania


UKATILIWA KUTUMIA NGUVU

zipo taarifa zinaonesha 61% ya wanawake walioko kanda ya kati hufanyiwa aina hii ya ukatili ,na 22% ya wanawake wa kanda ya kaskazini.


UKATILI WA KINGONO


taarifa zinaonesha kuwa ,mkoa wa mara unaongoza kwa 48.1%  na mikoa mingine ni kama ifuatavyo : kigoma (31.9%),mbeya (30.8%), ruvuma (30.4%) na rukwa (30.2%).


UKATILI WA KIUCHUM

32.56% ya wanawake wanakumbwa na ukatili huu ,kwa kunyimwa haki ya kumiliki ardhi na mali nyingine.


NANI HUFANYA UKATILI WA KIJINSIA?

ukatili wa kijinsia hufanywa na Baba , mama ,mke ,shemeji , baba mkwe, mama mkwe, shangazi, mjomba ,dada ,kaka, nk.
MAPENDEKEZO ILI KUONDOA UKATILI WA KIJINSIA

Tanzania imeridhia mikataba ya kimataifa inayopinga ukatili wa kijinsia .mikataba hii ni kama mkataba wa A frika wa haki za binadamu na haki za watu ,Mkataba wa Nyongeza wa haki za wanawake (2003) ,Mkataba
wa kuondoa .Aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake -CEDAW(1979),na mengineyo.hivyo basi ,ili kuweza kutekeleza mikataba hii na kuwalinda wanawake dhidi ya ukatili ,tanzania inatakiwa


  • .kutunga sheria ambayo itakataza itakataza ukatili wa kijinsia wa aina zote ikiwemo ukatili wa kutumia nguvu ,ngono,saikolojia nk kuunda vituo vya kuhifadhi waathirika wa ukatili .,
  • .Kuunda vituo vya ushauri nasaa wa kifamilia juu ya ukatili na kusaidia waatirika kurudi katika hali yao ya kawaida .
  • Kujenga mazingira ya kupewa msaada wa haraka kwa wahanga kwa kuanzisha ngazi za serikali za mitaa; vijiji mpaka serikali kuu,
  • Kuweka mifumo ya kuwapatia msaada wa sheria kwa wahanga wa ukatili n.k
  • Kutengeneza mazingira ya kuwaelimisha wanajamii wa marika yote madhara na athari za ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto wa kike
  • Kuanzisha jitihada za kutoa elimu katika ngazi zote na kuelezea umuhimu wa kuhelimisha haki za Binadamu na haki za wanawake kwa misingi ya kuondoa ukatili.

 

KERO KATIKATI YA JIJI LA MBEYA: MACHINGA WAJIACHIA WAPANGA BIDHAA MPAKA BARABARANI , WAHUSIKA WAMEUCHUNA, JE MAPATO HAYA YANAENDA WAPI? NA NI SAHIHI HAWA WATU KUWA HAPA?

Imekuwa ni moja ya kero kubwa na uchafuzi wa jiji katika Lango la Jiji eneo ambalo wageni , Viongozi wakubwa na watu mbalimbali wanapita.
Kero hii ambayo wahusika mnaliona hili na mnalikalia kimya linawapa watu maswali mengi sana na mpaka kudhania labda ni kamradi kamtu na ambako hakaeleweki eleweki kuwa pato lake linaenda wapi
Sio pengine ni kakipande tuu kutoka Eneo la Benki ya CRDB hadi Eneo la BP kona ya kuelekea Posta. Inafahamika kuwa eneo hili lilikatazwa kufanyika biashara lakini sasa imekuwa ndio eneo la watu kuweka Bidhaa zao na kila siku watu hawa wanazidi
Je Wahusika mpo na mnalizungumziaje?
 Hapa kila mtu anaweka Bidhaa zake wenye Nguo , Viatu na vitu mbalimbali wote wapo hapa
 Kila mmoja yupo Huru tuu
 Hapa ni nje ya wakusanya mapato(TRA) wanakazana kufukuza watu wengine maeneo mengine je hawa hawawaoni? 
 Pamegeuka Duka
 Kila kitu kinapatikana eneo hili
 Hii njia ya kuelekea Posta unakaribishwa na Viatu 
 Wengine ndio kwanza wanaanza weka mzigo
 Kila mmoja anawahi kuanza biashara
 Wale Mgambo wa Jiji ina maana hapa hawakupangiwa kupita?
 Wadau hili si ni Duka kabisa!
 Je sasa hapa hawa ni Machinga ama wafanya biashara?
Hata bei zao ukigusa hapa sio za Machinga....

Ndugu Mdau na Msomaji wa Mbeya yetu... Toa maoni yako Juu ya Hili...

Picha na Mbeya yetu

AGA KHAN YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KWA HOSPITALI ZA HALMASHAURI 4 ZA MBEYA‏

 Mwenyekiti wa kamati ya afya Aga Khan Mbeya (kushoto)Sultan Thawer, akitoa taarifa kabla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya tiba kwa Halmashauri nne za Mkoa wa Mbeya.
 Mwenyekiti wa kamati ya afya Aga Khan Mbeya (kushoto)Sultan Thawer, akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro kabla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya tiba kwa Halmashauri nne za Mkoa wa Mbeya.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro,akisaidiwa na Mganga mkuu wa Mkoa,Dk. Seif Mhina,Katibu tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja na Mwenyekiti wa Kamati ya afya Aga Khan Sultan Thawer wakikata utepe kuashiria kukabidhi msaada wa vifaa hivyo.
 Mwenyekiti wa kamati ya afya Aga Khan Mbeya,Sultan Thawer, akipongezwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro baada ya kukabidhi msaada.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiangalia baadhi ya vifaa vilivyotolewa na Hospitali ya Aga Khan.
 Meneja wa Hospitali ya Aga Khan Mbeya, Abel kide, ambaye pia ni mratibu wa Mradi wa tuunganishe mkono pamoja akimuonesha moja ya mashine mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro.
 Mkuu wa Mkoa na viongozi wa Aga Khan wakiangalia moja ya mashine zilizokabidhiwa kwa Halmashauri nne za Mkoa wa Mbeya.
Picha ya pamoja

HOSPITALI ya Aga khan ya Mbeya imetoa msaada wa vifaa tiba kwa Hospitali na vituo vya afya katika Halmashauri nne za Mkoa wa Mbeya vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 300.
Msaada huo ulikabidhiwa  na uongozi wa Hospitali hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro kwa niaba ya Halmashauri husika katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkapa uliopo Sokomatola jijini hapa.
Mratibu wa Mradi wa tuunganishe mkono pamoja(JHI) Mkoa wa Mbeya, Abel Kide, ambaye pia ni Meneja wa Hospitali ya Aga Khan alisema Halmashauri zilizonufaika na mradi huo ni pamoja na Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Kyela, Mbozi na Momba.
Kide alizitaja Hospitali na zahanati zinazopatiwa vifaa hivyo kuwa ni Zahanati ya Ngana na Hospitali ya Wilaya ya Kyela(Kyela), Zahanati ya Iyunga na kituo cha Afya Kiwanja Mpaka(Mbeya jiji), Hospitali ya Wilaya ya Mbozi(Vwawa)na Zahanati ya Ivuna iliyopo wilayani Momba.
Alivitaja vifaa hivyo kuwa ni Vitanda vya kujifungulia wajawazito, vitanda vya wagonjwa wa kawaida, Mashine za kuchemshia vifaa vya hospitalini, Mashine ya kumpa joto mtoto aliyetoka kuzaliwa, Mashine ya Ultra Sound,Mashine ya kumtolea uchafu mtoto mchanga,mashine za kupima uzito, joto, urefu na Presha na kwamba vyote jumla vinagharimu zaidi ya shilingi Milioni 300.
Kide alisema lengo la kutoa msaada huo ni kuboresha afya ya mama mjamzito, mtoto mchanga na mtoto aliyechini ya miaka mitano ikiwa ni pamoja na kusogeza huduma za afya  karibu na wananchi hususani kuokoa vifo vinavyotokea wakati wa kujifungua.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbasi Kandoro alipongeza Hospitali ya Aga Khani kwa Msaada waliotoa katika Halmashauri hizo na kuziomba taasisi zingine kuungana na Serikali katika mpango wa kuhakikisha vifo vya Wanawake wajawazito, watoto wachanga na waliochini ya umri wa miaka mitano vinapungua.
Kandoro alisema mkakati wa kupunguza vifo hivyo hautafanikiwa ikiwa utakuwa ukifanywa na sekta moja ya afya pekee bali kwa kushirikisha sekta zingine  binafsi za serikali, viongozi wa dini na vyombo vya habari.
Aliongeza kuwa ili kukomesha kabisa vifo hivyo, Halmashauri zitenge bajeti za kununua mfumo wa huduma tembezi(Mobile clinic) ili ziweze kufika hata maeneo ambayo hakuna huduma ya afya kwa kuwasogezea wananchi huduma ili waweze kupata msaada wa matibabu wakati wowote.
Sambamba na kupokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alizindua Mpango wa utekelezaji wa kupunguza kasi ya vifo vitokanavyo na matatizo ya uzazi, watoto na watoto waliochini ya umri wa miaka mitano.

Kandoro aliongeza kuwa mkakati huo ni maagizo ya Raisi wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Mkakati wa kitaifa uliofanyika Mei 15 Mwaka huu ambapo aliagiza Kila Mkuu wa Mkoa kuutafakari mkakati huo kulingana na mazingira wanakotoka.

TANGAZO

BIOLANDS YAKABIDHI MSAADA WA AMBULANCE NISSAN PATROL KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA KYELA.


Jukwaa ambapo sherehe ya Makabidhiano ilifanyika
Gari la Kubebea wagonjwa likiwa linaingia kwa ajili ya Makabidhiano
Meza kuu
 Meneja Mkuu msaidizi wa Biolands(Kulia) akimkabidhi na kupongezana  na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Ester Malenga ufunguo wa Gari la Wagonjwa katika Sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya Halmashauri ya Wilaya Kyela.
 Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Malenga akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Gari la Wagonjwa walilokabidhiwa na kampuni ya Biolands , akisaidiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Seif Mhina 
 Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Ester Malenga  akifungua Mlango wa Gari la Wagonjwa Kuashiria Uzinduzi 
Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Ester Malenga akiwasha Gari la wagonjwa 
 Meneja wa Biolands Tawi la Kyela Erasto Kilongo akisoma  Risala kwa Mgeni Rasmi kabla ya Makabidhiano ya Gari ya wagonjwa 
 Mwenyekiti wa Bodi ya uhamasishaji wa kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya (HIMSO) Dkt. Charles Mbwanji akitoa salamu za shirika lake katika sherehe za makabidhiano ya Gari 
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt Seif Mhina akizungumza wakati wa Sherehe za Makabidhiano ya Gari la wagonjwa
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Clemence Kasongo akitoa Shukurani kwa niaba ya watumishi wa Halmashauri Baada ya kukabidhiwa msaada wa Gari 
 Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Ester Malenga akitoa Hotuba yake kwa wageni waalikwa na wananchi wa Wilaya ya Kyela Baada ya Kukabidhiwa msaada wa Gari ya Wagonjwa na Biolands
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Gabriel Kipija akitoa shukurani za Halmashauri kwa kampuni ya Bioland baada ya kukabidhiwa Msaada wa Gari la Wagonjwa.
 Meneja Mkuu Msaidizi wa Biolands Felix Mtawa akitoa neno la utangulizi kabla ya Kukabidhi Msaada wa Gari ya Wagonjwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela
Wananchi na Wageni mbalimbali waliohudhuria Sherehe za makabidhiano ya Gari la wagonjwa wakifuatilia kwa makini tukio hilo

*****************

KAMPUNI ya Biolands International Ltd imetoa msaada wa gari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) aina ya Nissan Patrol kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela lenye thamani ya shilingi zaidi ya Milion 76.
Hafla ya makabidhiano ya gari hilo imefanyika  katika viwanja vya Halmashauri hiyo baina ya Mkuu wa Wilaya ya Kyela Magreth Esther Malenga, Meneja wa Bioland Felix Mtawa na Mwenyekiti wa uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya Afya, Dk.Charles Mbwaji wakishuhudiwa na mganga mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Seif Mhina.
Katika Risala ya Bioland iliyosomwa na Meneja wa Tawi, Erasto Kilongo, alisema lengo la msaada huo ni kutambua mchango wa wananchi katika maeneo wanayofanya kazi.
Alisema Bioland ni Kampuni Binafsi inayojishughulisha na ununuzi wa Kakao katika Wilaya za Kyela na Rungwe ambapo   inafanya kazi na na wakulima zaidi ya 20,000 katika vituo 137 vilivyopo katika wilaya hizo mbili.
Alisema Kampuni hiyo inafanya kazi moja kwa moja na wakulima katika kufanikisha shughuli za vyeti mbalimbali ambavyo vinasaidia kuwepo kwa uhakika wa soko la kakao, vyeti kama vile kilimo hai (organic farming), Kilimo endelevu (Rain forest Allience),na  Usawa wa kibiashara katika jamii (social and Fare Trade).
Alisema katika sekta ya Afya na usalama wa wazalishaji, Kampuni  imenuia kuhakikisha afya za wakulima na familia zao zinaendelea kuimarika wakati wote na kupata huduma za afya kwa gharama nafuu kupitia mradi wa Bima ya afya ya jamii.
Alisema  katika kufanikisha mradi huo, Kampuni  ilikubali kutenga kiasi cha dolla 60,000 za kimarekani kwa kipindi cha miaka 5 toka 2010 hadi 2014 kwa ajili ya kutoa ruzuku kwa wakulima wanaojiunga na bima ya afya ya jamii.
Aliongeza kuwa  Kutokana na umuhimu huu wa kuhakikasha afya za wakulima na familia zao zinaimarika pia Biolands imefadhili ununuzi wa gari la wagonjwa (Ambulance)  lenye thamani  Shilingi Milioni 76,140,000/=, ambalo  limekabidhiwa kwa Halmashauri kwa niaba ya CHIF, HIMSO, CIDR na wananchi wa Kyela.
Awali akitoa salamu kwa niaba ya HIMSO, Dk. Charles Mwanji, alisema kazi ya HIMSO ambalo ni shirika lisilokuwa la kiserikali ni kuhakikisha wananchi wanajiunga na mfuko wa jamii na kupata huduma ipasavyo.
Alisema moja ya majukumu yao ilikuwa ni kuwahamasisha Bioland kununua gari la wagonjwa kutokana na umuhimu kwa Wananchi wa Kyela ili waweze kupata huduma za mfuko wa bima kiufasaha.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dk. Seif Mhina, alisema Kazi ya Bioland na HIMSO ilikuwa ni kutoa gari hivyo Halmashauri ihakikishe gari linatumika katika shughuli iliyokusudiwa.
Alisema ili hayo yakamilike ni bora gari hilo likawa linashindwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kyela ili kuepuka matumizi tofauti ya gari kama ilivyowahi kutokea kwa magari mengine.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kyela ikishukuru kwa niaba ya Wananchi wa Wilaya ya Kyela, alisema Kampuni hiyo imemaliza kilio cha Wananchi wa Kyela cha kutaka gari la wagonjwa kilichokuwepo muda mrefu.
Alisema kupitia hamasa walioonesha Bioland Wilaya yake itaanza kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya ili kuhakikisha kila mwananchi anatumia kadi kwenye matibabu.
Aidha alitoa wito kwa watumishi wa vituo vya Afya na Mahospitali kutoa kipaumbele kwa wagonjwa wenye kadi kuliko wenye fedha mkononi ili wapate tiba kama serikali ilivyoagiza.