Monday, November 3, 2014

HISTORIA YA WANYAKYUSA

HISTORIA YA WANYAKYUSA
Historia inasema kwamba asili ya Wanyakyusa ni mkoani Morogoro. Kabila hilo likitokana na kabila la Waluguru. Hili hasa ndilo chimbuko la Wanyakyusa.

Inasemekana kwamba mwindaji mmoja wa Kiluguru alitembea peke yake porini bila ya kuongozana na mtu mwingine. Alitembea hadi akafika maeneo ya Kabale huko Suma, Tukuyu wilayani Rungwe. Akiwa huko, akaendelea na kazi yake ya uwindaji.
Baadaye akatokea Mzulu mmoja kutoka Afrika Kusini aliyekuwa na binti yake. Akafika maeneo alikokuwa akiishi yule mwindaji Mluguru, naye akapiga kambi hapo Kabale, wakaungana katika maisha ya uwindaji.

Ikawa kila yule Mluguru akitoka asubuhi kwenda kuwinda, alikuwa akifanikiwa kurejea nyumbani na wanyama wakati rafiki yake wa Kizulu alikuwa akirudi mikono mitupu.

Kutokana na hali hiyo, Mluguru akageuka kuwa mfadhili wa Mzulu, kwa kutoa misaada mara kwa mara, na kwa kulipa fadhila hizo, akamwoza bintiye kwa Mluguru.

Akamwoa na maisha yakaendelea huku nyumbani kwa mwindaji wa Kiluguru na mkewe binti wa Kizulu, kukiwa hakukosekani nyama kama kitoweo.

Kwa sababu ili kuihifadhi nyama ilibidi kwanza ibanikwe, basi kitendo hicho kilisababisha harufu nzuri ya kitoweo kile kusambaa eneo kubwa na kufika hadi ukweni kwake nyumbani kwa Mzulu. 
 Moja ya nyumba za asili za wanyakyusa

Ndipo Mzulu yule akawa anasema mara kwa mara: “Pale panatoa kyusi kila siku” akimaanisha moshi kwa lafudhi ya lugha ya kwao.

Mazoea ya kutamka ‘kyusi’ kila siku, yakaligeuza neno ‘kyusi’ na sasa likawa linatamkwa ‘kyusa’, baadaye ‘kyusa’ ilipozidi kutamkwa kwa mara nyingi, nayo pia ikabadilika bila kukusudia ndipo watu walipokuwa wakimwita Mluguru ‘Mnyakyusa’, kwa kuwa moshi ukiambatana na harufu ulikuwa ukitokea ndani ya nyumba yake na kusambaa.

Kwa hiyo, tangu hapo na kutokana na jina hilo alilopewa kwa ajili ya mazoea ya kukosea kutamka kitu, hata watoto wake pia waliozaliwa na Mluguru na mkewe Mzulu, wakawa wakiitwa ‘Wanyakyusa’.

Hiyo ndiyo asili na chimbuko la kabila la Wanyakyusa, na kwa kuwa Mnyakyusa alikuwa tayari ana asili ya pande mbili - wakati baba akiwa na asili ya Kiluguru na mama Mzulu wa ‘kwa Madiba’.

Na hata uchifu ukaanzia mahali pale palipokuwa panaitwa Kabale, na yule Mluguru aliupata uchifu kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa mwanzilishi na mkazi wa kwanza wa eneo lile na ndiye aliyekuwa anafahamika zaidi.

Mavazi yao

Kwa upande wa mavazi, Wanyakyusa walikuwa wakivaa mavazi yaliyokuwa yakijulikana kama ‘Lyabi’, Ni mavazi ya kwanza kwa kabila yakivaliwa enzi za utumwa. Mavazi haya ni yale yanayofunika maeneo ya siri pekee, na kwa wale ‘waheshimiwa’, kidogo basi wao walivaa vazi lililokuwa likiitwa ‘kikwembe’ au ‘kilundo’.

Mavazi haya yaliyovaliwa kwa mtindo kama lubega, ndiyo yaliyomtambulisha na kumtofautisha mhusika mbele ya jamii.

Ngoma yao

Ngoma iliyokuwa ikichezwa na Wanyakyusa enzi hizo, ilikuwa ni ya kuchezea mikuki na mara nyingi ngoma hiyo ilikuwa ikichezwa wakati wa msiba.

Lakini ngoma za kawaida zilizokuwa zikichezwa pasipo kutumia mikuki na wakati wa sherehe na shughuli nyingine, ni ‘Ipenenga’. Hii mara nyingi ilikuwa ikichezwa na watu ‘wastahiki’ tena kwa madaha na maringo ya hali ya juu. Hata machifu walikuwa wakiicheza sana ngoma hii.

Chakula chao

Chakula chao kikuu na ambacho Mnyakyusa angeonekana kuwa amemkarimu mgeni, si kingine bali ni dizi zinazomenywa na kupikwa maarufu kama ‘mbalaga’.

Mnyakyusa halisi kama atakula chakula lakini akakosa ‘mbalaga’ hujiona kama bado hajakamilisha mlo, ingawaje siku hizi kuna mabadiliko fulani ambayo wengi hupendelea ugali na wali; lakini bado asili ya chakula chao hawawezi kuibadilisha kamwe.

Na ni lazima chakula kama ‘kande’ kipikwe kwenye tukio la msiba uwao wote, kama shughuli za msiba zitakwisha pasipo kupikwa chakula hicho chenye mchanganyiko wa mahindi na maharage; msiba huwa haujakamilika hata kama wafiwa ni watu wenye kujiweza kifedha zaidi lakini ni lazima kande zitapikwa japo kiasi.

Utamaduni wao
Kwa kawaida Wanyakyusa hawana mambo ya unyago kama ilivyo kwa baadhi ya makabila hapa nchini. Wao hawapendelei kabisa mila na desturi za kuwaweka mabinti ndani au kuwafanyia mambo yoyote ya tohara.

Hii ni pamoja na upande wa vijana wa kiume ambao nao hawafanyiwi ya tohara kama makabila mengine isipokuwa tu kwa upande wa vijana wa kiume mara tu wanapotimiza umri wa miaka 13 na kuendelea.

Hawa wazazi wao wa kiume huwatengea eneo ambalo kijana hutakiwa kujifunza kujitegemea akiwa bado mbichi. Hapo hutakiwa kuwa na kibanda chake na kuhama kutoka nyumba moja na wazazi wake
Chanzo: SAUTI YA VIJANA BUSOKELO

MLIMA RUNGWE



Mlima rungwe ni mlima ulipopo katika wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, Inaaminika kwamba mlima huu ulitokana  na volcano iliyozimika kusini kusini magharibi mwa Tanzania,  Ikikadiriwa ya kwamba mlipuko wake wa mwisho ulitokea mnamo miaka 2000 hadi 5000 iliyopita. Ukiwa na kimo cha 2960 m ni mlima mkubwa kusini mwa Tanzania na ni wa tatu kwa ukubwa Tanzania
 Mlima Rungwe

 Mlima Rungwe ukionekana kwa mbali kama picha ilivyochukuliwa kutoka The green city Profile

Mlima unasimama juu ya ncha ya kaskazini ya Ziwa nyasa. Upande wa kusini-mashariki wa mlima hupokea usimbishaji wa 3,000 mm kwa mwaka ambao ni juu kabisa katika Tanzania.

Mazingira ya mlima ni nchi yenye rutba na kilimo. Rungwe ni eneo la Wanyakyusa.Jina la mlima limekuwa pia jina la wilaya ya Rungwe

 Katika mlima rungwe kuna viumbe hai mbali mbali kama ndege na wanyama. Moja ya wanyama wanaopatikana katika mlima rungwe ni nyani ambapo kuna aina moja ya nyani wanaopatikana mlimani hapo tu ambao wanajulikana kama kipunji.
Nyani aina ya kipunji wanaopatikana mlima Rungwe tu

 


Ukiwa juu yam lima rungwe unaweza kuliona ziwa nyasa vizuri pamoja na mbuga ya wanyama kitulo. Upande wa kusini mwa mlima utaona ziwa nyasa na upande wa mashariki utaona bonde la kitulo.
 Ziwa Nyasa
Kitulo National Park

HIKI NDO KIMONDO KILICHODONDOKA MBOZI TANZANIA

Kimondo ambacho kilidondoka kutoka angani huko Mbozi mbeya karibu na mji wa vwawa.Kinakadiriwa kuwa na uzito wa tani 12 na kilianguka katika mlima wa mlenje

Kimondo hicho ni kimoja kati ya vimondo 10 vinavyojulikana duniani na kina urefu wa mita 3.3 na urefu wa mita 1.63 na kimo cha 1.22.

Kwa upande wa umbile kimondo hichi kiko tofauti na vimondo vingine vinavyopatikana ulimwenguni kwa sababu kimondo hichi ni hasa kwa chuma. Chuma kimechukua asilimia 90.45 na nikel asilimia 8.69, sulfuri asilimia 0.01 na fosfori asilimia 0.11 ya masi yake

Maporomoko ya Malasusa

Malasusa falls
Maajabu mengi yaliyopo Tukuyu mkoani mbeya ni maporomoko ya Malasusa . ukiwa unaelekea kwenye maporomoko ya Malasusa utasikia
maporomoko  kwa mbali kabla hujafika kwenye maporomoko yenyewe na ni moja kati ya maporomoko mazuri katika ukanda wa nyanda za juu kusini
 Maporomoko ya Malasusa kama picha ilivyochukuliwa na Emwandosya

MKURUGENZI, WANAHABARI NA WANANCHI MBEYA, KUISAFISHA MBALIZI

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbeya, Upendo Sanga
MKURUGENZI wa halmashauri ya Mbeya, Upendo Sanga, baadhi ya wanahabari mkoani Mbeya, wananchi na wakuu wa idara za Halmashauri hiyo, wanatarajia kuongoza kampeni endelevu ya kuuweka safi mji wa Mbalizi wilayani humo na kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira.


Kampeni hiyo ya usafi, inaratibiwa na kikundi cha Vijana wanaofanya kazi ya kutunza na kuhifadhi mazingira kwa kujitolea mkoani hapa, wanaojulikana kwa jina la Vijana wazalendo Mbalizi(UVIWAMBA).


Akizungumza na waandsishi wa habari jana, mratibu wa kikundi hicho, Gordon Kalulunga, alisema kuwa, itakuwa mara ya pili kwa Mkurugenzi huyo na baadhi ya waandishi wa habari kuungana na juhudi za vijana wanaojitolea kufanya usafi katika mji huo.


“Ni faraja kubwa sana kwetu kuona Halmashauri yetu inaungana nasi katika kutimiza wajibu wetu kwa taifa, hasa tunapoona Mkurugenzi na waandishi wa habari wanakuja huku chini na kuona umuhimu wa kutoa support kwa kada ya watu tunaoamua kujitolea” alisema Kalulunga.


Alisema usafi huo utafanyika katika eneo la makao makuu ya Kanisa la Uinjilisti Tanzania mpaka eneo la stendi ya Umalila, na kuhitimishwa kwa kubadilishana mawazo endelevu ya usafi katika mji huo wa Mbalizi kati ya wananchi watakaojitokeza na wageni watakaoongozwa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo.


Naye makamu Mwenyekiti wa kikundi hicho, Ayas Yusuph, alisema kikundi chao kinafanya usafi kila siku ya Juma mosi ya juma kwa kushirikiana na baadhi ya wananchi wa mji huo.


“Mkurugenzi kuungana nasi ni jambo kubwa sana ambalo linatuongezea hamasa ya kuendelea kujitolea na hivi sasa tayari tumebandika matangazo kwa ajili ya kuwaeleza wananchi wenzetu kuwa kila mmoja siku hiyo afanye usafi kwa hiari katika makazi na maeneo anayofanyia kazi’’ alisema Ayasi.


Kwa upande wake Mkurugenzi Upendo Sanga, alisema, ataungana na vijana hao pamoja na baadhi ya wakuu wa idara ya mazingira, kufanya usafi katika mji huo ambao ni kioo cha wilaya na mkoa wa Mbeya kwa wageni wanaotumia usafiri wa ndege wa kimataifa wa Songwe.


“Nitashiriki katika zoezi hilo la usafi siku ya Jumamosi. Ni wajibu wangu na wananchi wote, maana Mbalizi ni kioo cha mkoa wa Mbeya kupitia uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Songwe, ambao upo katika wilaya yetu na mgeni yeyote anayetaka kwenda katikati ya Jiji la Mbeya, lazima apite Mbalizi” alisema Upendo Sanga.

 AKISHIRIKI KUZIBUA MIFEREJI NA VIJANA WA MBALIZI AMBAO WAMEJITOLEA KUFANYA USAFI KATIKA MJI HUO.

 AKIWA NA VIJANA ENEO LA KAZI MBALIZI MWAKA JANA 2013.

Kushirki katika kazi hiyo ya usafi kwa Mkurugenzi huyo, kutakuwa kwa awamu ya pili, ambapo awali mwaka jana, alishiriki katika kuzibua baadhi ya mitaro iliyokuwa imeziba katika stendi kuu ya wilaya hiyo, iliyopo eneo la Tarafani katika mji wa Mbalizi.


Kwa sasa Serikali, inaendelea kukamilisha ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami katika mji huo.

0 comments:

Post a Comment