Jukwaa ambapo sherehe ya Makabidhiano ilifanyika
Gari la Kubebea wagonjwa likiwa linaingia kwa ajili ya Makabidhiano
Meza kuu
Meneja
Mkuu msaidizi wa Biolands(Kulia) akimkabidhi na kupongezana na Mkuu wa
Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Ester Malenga ufunguo wa Gari la Wagonjwa
katika Sherehe zilizofanyika kwenye viwanja vya Halmashauri ya Wilaya
Kyela.
Mkuu
wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Malenga akikata utepe kuashiria uzinduzi
wa Gari la Wagonjwa walilokabidhiwa na kampuni ya Biolands , akisaidiwa
na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Seif Mhina
Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Ester Malenga akifungua Mlango wa Gari la Wagonjwa Kuashiria Uzinduzi
Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Ester Malenga akiwasha Gari la wagonjwa
Meneja wa Biolands Tawi la Kyela Erasto Kilongo akisoma Risala kwa Mgeni Rasmi kabla ya Makabidhiano ya Gari ya wagonjwa
Mwenyekiti
wa Bodi ya uhamasishaji wa kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya (HIMSO)
Dkt. Charles Mbwanji akitoa salamu za shirika lake katika sherehe za
makabidhiano ya Gari
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt Seif Mhina akizungumza wakati wa Sherehe za Makabidhiano ya Gari la wagonjwa
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Clemence Kasongo akitoa
Shukurani kwa niaba ya watumishi wa Halmashauri Baada ya kukabidhiwa
msaada wa Gari
Mkuu
wa Wilaya ya Kyela Mh. Magreth Ester Malenga akitoa Hotuba yake kwa
wageni waalikwa na wananchi wa Wilaya ya Kyela Baada ya Kukabidhiwa
msaada wa Gari ya Wagonjwa na Biolands
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Gabriel Kipija akitoa shukurani za
Halmashauri kwa kampuni ya Bioland baada ya kukabidhiwa Msaada wa Gari
la Wagonjwa.
Meneja
Mkuu Msaidizi wa Biolands Felix Mtawa akitoa neno la utangulizi kabla
ya Kukabidhi Msaada wa Gari ya Wagonjwa wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kyela
Wananchi na Wageni mbalimbali waliohudhuria Sherehe za makabidhiano ya Gari la wagonjwa wakifuatilia kwa makini tukio hilo
*****************
KAMPUNI ya Biolands
International Ltd imetoa msaada wa gari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) aina ya
Nissan Patrol kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela lenye thamani ya shilingi
zaidi ya Milion 76.
Hafla ya makabidhiano ya gari
hilo imefanyika katika viwanja vya
Halmashauri hiyo baina ya Mkuu wa Wilaya ya Kyela Magreth Esther Malenga,
Meneja wa Bioland Felix Mtawa na Mwenyekiti wa uhamasishaji wananchi kujiunga
na mfuko wa bima ya Afya, Dk.Charles Mbwaji wakishuhudiwa na mganga mkuu wa
Mkoa wa Mbeya, Dk. Seif Mhina.
Katika Risala ya Bioland
iliyosomwa na Meneja wa Tawi, Erasto Kilongo, alisema lengo la msaada huo ni
kutambua mchango wa wananchi katika maeneo wanayofanya kazi.
Alisema Bioland ni Kampuni Binafsi
inayojishughulisha na ununuzi wa Kakao katika Wilaya za Kyela na Rungwe ambapo inafanya kazi na na wakulima zaidi ya 20,000
katika vituo 137 vilivyopo katika wilaya hizo mbili.
Alisema Kampuni hiyo inafanya kazi
moja kwa moja na wakulima katika kufanikisha shughuli za vyeti mbalimbali
ambavyo vinasaidia kuwepo kwa uhakika wa soko la kakao, vyeti kama vile kilimo hai
(organic farming), Kilimo endelevu (Rain forest Allience),na Usawa wa kibiashara katika jamii (social and
Fare Trade).
Alisema katika sekta ya Afya na
usalama wa wazalishaji, Kampuni imenuia
kuhakikisha afya za wakulima na familia zao zinaendelea kuimarika wakati wote
na kupata huduma za afya kwa gharama nafuu kupitia mradi wa Bima ya afya ya
jamii.
Alisema katika kufanikisha mradi huo, Kampuni ilikubali kutenga kiasi cha dolla 60,000 za
kimarekani kwa kipindi cha miaka 5 toka 2010 hadi 2014 kwa ajili ya kutoa
ruzuku kwa wakulima wanaojiunga na bima ya afya ya jamii.
Aliongeza kuwa Kutokana na umuhimu huu wa kuhakikasha afya za
wakulima na familia zao zinaimarika pia Biolands imefadhili ununuzi wa gari la
wagonjwa (Ambulance) lenye thamani Shilingi Milioni 76,140,000/=, ambalo limekabidhiwa kwa Halmashauri kwa niaba ya
CHIF, HIMSO, CIDR na wananchi wa Kyela.
Awali akitoa salamu kwa niaba
ya HIMSO, Dk. Charles Mwanji, alisema kazi ya HIMSO ambalo ni shirika
lisilokuwa la kiserikali ni kuhakikisha wananchi wanajiunga na mfuko wa jamii
na kupata huduma ipasavyo.
Alisema moja ya majukumu yao
ilikuwa ni kuwahamasisha Bioland kununua gari la wagonjwa kutokana na umuhimu
kwa Wananchi wa Kyela ili waweze kupata huduma za mfuko wa bima kiufasaha.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya, Dk. Seif Mhina, alisema Kazi ya Bioland na HIMSO ilikuwa ni kutoa gari
hivyo Halmashauri ihakikishe gari linatumika katika shughuli iliyokusudiwa.
Alisema ili hayo yakamilike ni
bora gari hilo likawa linashindwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kyela ili
kuepuka matumizi tofauti ya gari kama ilivyowahi kutokea kwa magari mengine.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya
ya Kyela ikishukuru kwa niaba ya Wananchi wa Wilaya ya Kyela, alisema Kampuni
hiyo imemaliza kilio cha Wananchi wa Kyela cha kutaka gari la wagonjwa
kilichokuwepo muda mrefu.
Alisema kupitia hamasa
walioonesha Bioland Wilaya yake itaanza kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko
wa bima ya afya ili kuhakikisha kila mwananchi anatumia kadi kwenye matibabu.
0 comments:
Post a Comment