Mwenyekiti
wa kamati ya afya Aga Khan Mbeya (kushoto)Sultan Thawer, akitoa taarifa
kabla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya tiba kwa Halmashauri nne za Mkoa
wa Mbeya.
Mwenyekiti
wa kamati ya afya Aga Khan Mbeya (kushoto)Sultan Thawer, akitoa taarifa
kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro kabla ya kukabidhi msaada wa
vifaa vya tiba kwa Halmashauri nne za Mkoa wa Mbeya.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro,akisaidiwa na Mganga mkuu wa Mkoa,Dk.
Seif Mhina,Katibu tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja na Mwenyekiti wa
Kamati ya afya Aga Khan Sultan Thawer wakikata utepe kuashiria
kukabidhi msaada wa vifaa hivyo.
Mwenyekiti
wa kamati ya afya Aga Khan Mbeya,Sultan Thawer, akipongezwa na Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro baada ya kukabidhi msaada.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akiangalia baadhi ya vifaa vilivyotolewa na Hospitali ya Aga Khan.
Meneja
wa Hospitali ya Aga Khan Mbeya, Abel kide, ambaye pia ni mratibu wa
Mradi wa tuunganishe mkono pamoja akimuonesha moja ya mashine mkuu wa
Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro.
Mkuu wa Mkoa na viongozi wa Aga Khan wakiangalia moja ya mashine zilizokabidhiwa kwa Halmashauri nne za Mkoa wa Mbeya.
Picha ya pamoja
HOSPITALI ya Aga khan ya Mbeya
imetoa msaada wa vifaa tiba kwa Hospitali na vituo vya afya katika Halmashauri
nne za Mkoa wa Mbeya vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 300.
Msaada huo ulikabidhiwa na
uongozi wa Hospitali hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro kwa niaba ya
Halmashauri husika katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkapa
uliopo Sokomatola jijini hapa.
Mratibu wa Mradi wa tuunganishe
mkono pamoja(JHI) Mkoa wa Mbeya, Abel Kide, ambaye pia ni Meneja wa Hospitali
ya Aga Khan alisema Halmashauri zilizonufaika na mradi huo ni pamoja na
Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Kyela, Mbozi na Momba.
Kide alizitaja Hospitali na
zahanati zinazopatiwa vifaa hivyo kuwa ni Zahanati ya Ngana na Hospitali ya
Wilaya ya Kyela(Kyela), Zahanati ya Iyunga na kituo cha Afya Kiwanja Mpaka(Mbeya
jiji), Hospitali ya Wilaya ya Mbozi(Vwawa)na Zahanati ya Ivuna iliyopo wilayani
Momba.
Alivitaja vifaa hivyo kuwa ni
Vitanda vya kujifungulia wajawazito, vitanda vya wagonjwa wa kawaida, Mashine
za kuchemshia vifaa vya hospitalini, Mashine ya kumpa joto mtoto aliyetoka
kuzaliwa, Mashine ya Ultra Sound,Mashine ya kumtolea uchafu mtoto
mchanga,mashine za kupima uzito, joto, urefu na Presha na kwamba vyote jumla
vinagharimu zaidi ya shilingi Milioni 300.
Kide alisema lengo la kutoa
msaada huo ni kuboresha afya ya mama mjamzito, mtoto mchanga na mtoto
aliyechini ya miaka mitano ikiwa ni pamoja na kusogeza huduma za afya karibu na wananchi hususani kuokoa vifo
vinavyotokea wakati wa kujifungua.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya, Abbasi Kandoro alipongeza Hospitali ya Aga Khani kwa Msaada waliotoa
katika Halmashauri hizo na kuziomba taasisi zingine kuungana na Serikali katika
mpango wa kuhakikisha vifo vya Wanawake wajawazito, watoto wachanga na
waliochini ya umri wa miaka mitano vinapungua.
Kandoro alisema mkakati wa
kupunguza vifo hivyo hautafanikiwa ikiwa utakuwa ukifanywa na sekta moja ya
afya pekee bali kwa kushirikisha sekta zingine
binafsi za serikali, viongozi wa dini na vyombo vya habari.
Aliongeza kuwa ili kukomesha
kabisa vifo hivyo, Halmashauri zitenge bajeti za kununua mfumo wa huduma
tembezi(Mobile clinic) ili ziweze kufika hata maeneo ambayo hakuna huduma ya
afya kwa kuwasogezea wananchi huduma ili waweze kupata msaada wa matibabu
wakati wowote.
Sambamba na kupokea msaada huo
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alizindua Mpango wa utekelezaji wa kupunguza kasi ya vifo
vitokanavyo na matatizo ya uzazi, watoto na watoto waliochini ya umri wa miaka
mitano.
Kandoro aliongeza kuwa mkakati
huo ni maagizo ya Raisi wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Mkakati wa kitaifa
uliofanyika Mei 15 Mwaka huu ambapo aliagiza Kila Mkuu wa Mkoa kuutafakari
mkakati huo kulingana na mazingira wanakotoka.
0 comments:
Post a Comment